WAUZAJI WA KOROSHO (CASHEW NUTS) DARAJA LA KWANZA

Kutoka Green Resources Supply, tunawaletea korosho bora kabisa zilizoandaliwa kwa ubora wa Kimataifa, hizi ndizo faida za kula korosho:


KINGA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO
Siyo tu kwamba korosho zina kiwango kidogo cha mafuta (fat), lakini pia zina aina ya mafuta (Monounsaturated Fats) ambayo hutoa kinga kwenye moyo, aina ambayo huweza pia kupatikana kwenye Olive Oil.

Aidha, ndani ya korosho, kuna kirutubisho aina ya Oleic Acid ambacho utafiti unaonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha afya njema ya moyo na huwafaa hata wagonjwa wa kisukari.

Kama kweli unajali sana afya ya moyo wako, basi pendelea kula korosho za kila aina. Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya virutubisho nchini Uingereza (British Journal of Nutrition), umeonesha kuwa watu waliopendelea kula korosho na bidhaa zake, kama butter, idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo vilipungua kati ya asilimia 11 na 19.

Utafiti huo umeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa watu wanaotumia korosho angalau mara nne kwa wiki, walionesha kuondokewa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (coronary disease) kwa asilimia 37! Na iwapo mtu atakula sana korosho, hatari ya kupatwa na magonjwa huendelea kupungua zaidi.

Dondoo moja ya ulaji korosho na kujiepusha na magonjwa ya moyo yote mawili (coronary na cardiovascular), inasema kuwa chukua kiganja kimoja cha korosho tafuna au kijiko kimoja cha chakula kilicho jaa ‘nut butter’, kula hivyo mara nne kwa wiki.


MADINI YA COPPER, UIMARISHAJI MIFUPA, NISHATI
Licha ya kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, korosho pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya copper ambayo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Halikadhalika, korosho ina madini yanayoimarisha mifupa na kinga ya mwili.

KOROSHO NA UZITO
Kuna imani potofu kuwa kwa kuwa korosho ina mafuta, ukipenda kuzila basi mlaji huenda akanenepa. Imani hiyo si ya kweli kwani utafiti unaonesha kuwa watu wanaopenda kula korosho, angalau mara mbili kwa wiki, hakuna uwezekano wa kuongezeka uzito na badala yake wanaweza kupungua.

Hivyo inashauriwa kupenda kula korosho au butter kwa afya zetu na wala hakuna haja ya kuhofia kuongezeka uzito, badala yaje mlaji ndiye atakaepungua uzito. Elewa kwamba korosho kwa ujumla, ni chanzo kizuri cha madini ya copper, magnesium na phosphorus.

Green Resources Supply tunaandaa korosho kwa kuzingatia ubora wa Kimataifa:
KOROSHO KUTOKA GREEN RESOUCES SUPPLY ZIKIWA KATIKA PAKITI YAKE

KOROSHO KUTOKA GREEN RESOUCES SUPPLY ZIKIWA KATIKA PAKITI YAKE

PATA KOROSHO BORA KWA UBORA WA KIMATAIFA KUTOKA MTWARA!!


Kwa wateja ambao wanahitaji korosho zilizokwisha kuandaliwa tafadhali wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo hapo chini:


THE GREEN RESOURCE SUPPLY.
P.O. BOX 1095, MTWARA – TANZANIA.
TELEPHONE: +255 625 520 450
                      +255 625 576 434
MOBILE NO:  +255 656 510 914

Comments

Popular posts from this blog

MCHAI CHAI: SULUHISHO LA MATUMIZI YA MAJANI YA CHAI

GREEN RESOURCES: WAUZAJI WA ROZELA (ROSELLA)