UFUGAJI WA SUNGURA
Ufugaji wa sungura ni moja wapo ya chanzo kizuri cha mapato nchini Tanzania kama
watanzania watafanya yafuatayo,
- Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji.
- Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa sungura.
- Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi.
- Hulka ya uvumilivu na kuthubutu.
- Malengo thabiti ya ufugaji wa sungura.
- Tathmini ya soko la bidhaa za sungura.
- Kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa sungura.
Hivyo Kabla hujaamua kufuga sungura unatakiwa hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda
wa kuwahudumia wanyama kwani sungura wanahitaji uangalizi na hasa kwenye usafi kwa
sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu.
FAIDA ZA UFUGAJI WA SUNGURA
- Uzalishaji wa nyama
- Chanzo cha mapato
- Huzalisha ngozi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za binadamu kama vile kutengeneza viatu.
- Huzalisha mbolea kwa ajili ya matumizi ya shambani
- Mkojo wa sungura hutumika kutengeneza mbolea.
- Sungura huweza kutumika kwa ajili ya maonesho
UFUGAJI WA SUNGURA.
Kitaalam mtu yeyote anaepanga kuanzisha mradi wa ufugaji wa sungura anatakiwa kuwa makini
na mambo yafuatayo:
1. Aina ya sungura.
Kufahamu aina ya sungura anayotaka kufuga na yenye kuendana na mazingira anayoishi maana
kuna aina nyingi za sungura wafugwao duniani
2. Hali ya hewa ya eneo unalotaka kufugia.
Hapa tunaangalia zaidi katika unyevunyevu na joto katika eneo husika. Hivyo sehemu nzuri kwa
ajili ya kuzalishia sungura ni sehemu yenye joto la wastani 26oC-27oC ambayo itawafanya
wakue kwa afya njema.
3. Lishe
Suala la lishe linachukua asilimia 70-80 katika ukuaji wa sungura Hivyo ulishaji wa chakula bora
kwa sungura huleta mabadiliko makubwa katika ukuaji wao na lishe mbaya huwafanya
kutokuwa na afya bora na ukuaji wao huzorota.Sungura hupendelea zaidi majani na chakula cha
kuchanganya kwa kuzingatia mahitaji yao.
4. Magonjwa
Kama walivyo wanyama wengine sungura nao hushambuliwa na magonjwa pamoja na viroboto
ambayo husababisha kuzorota kwa ukuaji wa sungura na inaweza kusababisha hadi kifo. Mfano
wa magonjwa ambayo mara kwa mara huwasumbua sungura ni koksidiosis, “enteritis” na
“pasteurellosis”.
5. Ufahamu juu ya ufugaji wa sungura.
Ufugaji wa sungura una taratibu zake na zinatakiwa kufuatwa ili kuw ana matokeo bora katika
shughuli yote ya ufugaji wa sungura. Hivyo mfugaji anatakiwa kufahamu mbinu zote kuanzia
anapomleta sungura bandani mpaka anapoenda kumuuza.
Ni matumaini yangu kuwa wewe mfugaji mtarajiwa hata wewe ambaye tayari umeshaanza
kufuga umeweza kufaidika na kujifunza mbinu muhimu unazopaswa kuzitambua kabla ya
kuanza mradi wa kufuga sungura, ukiweza kuzizingatia mbinu hizo utaweza kujikomboa wewe
na familia yako lakini pia utawakomboa watanzania katika suala la ajira. Usikose kuungana na
mwandishi wa makala hii katika sehemu ya pili ambayo itazungumzia “Aina za sungura
wanaofaa kufugwa Tanzania pamoja na maeneo sahihi kwa ajili ya ufugaji wa sungura”.
Kwa wanaohitaji kuanza kufuga sungura na kujifunza zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo:
THE GREEN RESOURCE SUPPLY.
P.O. BOX 1095, MTWARA – TANZANIA.
TELEPHONE: +255 625 520 450
+255 625 576 434
MOBILE NO:
+255 656 510 914
E-MAIL: aneth.greenresouce@gmail.com
Comments