UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI
Kuku wa kienyeji ni wazuri kwa ufugaji kwa sababu: Wanavumilia sana magonjwa, Ni rahisi kuwahudumia, Chakula chao ni cha bei ya chini, Wavumilivu wa hali tofauti za hewa, Hawahitaji uangalizi wa karibu, na soko lake ni kubwa sana na bei nzuri (Mayai trei moja SHs 10,000 mpaka 15,000, kuku wakubwa wanaanzia SHs 15,000 mpaka 30,000). Hii haimaanishi kwamba, uwaache kuku bila uangalizi, kwani nao hupata magonjwa kama wasipo patiwa chanjo sahihi, hupungua uzito na uzalishaji mayai hushuka kama wasipo patiwa chakula chenye virutubisho vyote. Hapa naelezea vitu muhimu katika hii formula ya ufugaji kuku wa kienyeji kwa mafanikio: 1. Aina ya kuku: Chagua aina ya kuku wenye uwezo wa kutaga mayai mengi na wakati huohuo, kuzalisha nyama nyingi. Hii itakupa faida kote, kwenye upande wa nyama na upande wa mayai. Kuku hawa wanajulikana kama Chotara, wanatabia sawa na kuku wa kienyeji wenye asili ya Tanzania wanaopatikana maeneo mengi nchini; kutokana na uvumilivu wao wa magonjwa na hali tofauti